Karibu Afrika MasharikiK aribu Ukurasa wa Afrika Mashariki. Ingawa mimi si Mwafrika, ningependa kuwaonyesha watu wowote ulimwenguni mambo ya aina nyingi ambayo ninavyojua juu ya Afrika Mashariki. Kuna sababu kwa nini ninatengeneza huo ukurasa. Ya kwanza ni nilitaka kupatisha ukurasa ulioandikwa na lugha ya Kiswahili. Labda mnajua kuna kurasa nyingi zinazotengenezwa na Watanzania au Wakenya katika Internet, lakini zote zinaandikwa kwa Kiingereza tu. Kwa nini hawatumii lugha zao? Kwa hivyo mimi nimekata shauri kuunda ukurasa huu kwa lugha ya Kiswahili, ingawa sijui Kiswahili sana. Mimi nilipendelea kusafiri kokote ulimwenguni. Nilisafiri nchini nyingi kama Afrika Mashariki, Marekani, Mexico, Ulaya, India na Pakistan, China, Korea na Asia Kusini Mashariki n.k. Nilitembelea mijini kutafuta vitu na kuzungumza na wananchi huko. Watu wowote wanatofautiana na tena kulingana nao, nilivyofundishwa nao. Kama dini gani wangeamini, nyumbani gani wangeishi, tunaweza kuwa marafiki zao ikiwa tunataka kuwa. Miaka hii sisafiri nchi za kigeni. Kutumia Internet kunaniwezesha kujifunza habari za kigeni bila kwenda huko. Tunaweza kupeleka barua ya Internet kwenda kwa nchi yoyote katika dakika nusu. Tunaweza kupata marafiki zetu ulimwenguni. Nimepata barua kutoka marafiki Waafrika Mashariki pia. Ningependa kujua mambo mengi zaidi juu ya nchi zao, na ningekuwa na furaha nyingi kuwajibu maswali ya aina yoyote wakiniuliza. Kwa hivyo nimetengeneza ukurasa wa mawasiliano. Ningependa kupatia marafiki nyingi ulimwenguni na kujuliana na kuandikiana nao.
UGANDA ![]()
KENYA ![]()
Nilisafiri na marafiki zangu kaskazini ya Kenya kwa pikipiki ili kuona wanyama kama vile simba, tembo n.k. Lakini sikuona wao hata kidogo. Niliona punda milia tu. Nilifikiri kabisa hakuna wanyama wengi kasikazini ya Kenya. Ni kweli kuna tembo na simba huko kama mzee mwenyeji huko alituambia "Kuunaa weengii"? TANZANIA ![]()
Mjini Dar Es Salaam nilipendelea kula chakula cha aina nyingi cha Kiafrika Mashariki. Baadhi ya chakula ilikuwa ni ya Kihindi kama samosa na chai, ya Kiarabu kama pilau, na ya Kiingereza kama samaki na viazi, au ya mchanganyiko. Sikuzote nilikula matunda mengi na kunywa maji ya matunda mengi pia. UJAPANI ![]()
Hali ya hewa leo katika Ujapani:
![]() Wageni hao walikuwa wanafunzi Wakenya. Labda walikaribishwa na serikali ya Kijapani wakakuja na wakaishi huku kwa muda. Siku moja walikuja chuo kikuuni chetu na walituonyesha kucheza ngoma na nyimbo nzuri za Kenya. Baadaye walituambia mambo fulani juu ya Kenya na Afrika Mashariki kwa Kiingereza. Nilikuwa na nafasi nzuri ya kuzungumza nao, lakini sikuweza kusema maneno hata kidogo. Vijana Wajapani wengine wengi walikuwa pia ni kimya tu. Wakenya wote walisema mengi. Kwa hivyo walionekana walifikiria kwamba sisi vijana Wajapani hatujui Kiingereza au hatuna neno katika mazungumzo na wageni. Lakini si kweli. Wageni hao walitueleza kwamba watu wa Afrika Mashariki wanaelekea utamaduni wa Kizungu hasa wa Kiingereza. Kwa hivyo utamaduni wa Kijapani au Kiasia ulionekana kwao ni ya kigeni sana. Walisema wanatofautiana na Wajapani mahali popote wakati kokote. Maana yake ni hawakupendelea kukaa huku Ujapani wakila chakula cha Kijapani, wakisikilia muziki ya Kijapani au wakiona picha ya Kijapani. Miaka fulani baadaye nilitembea bara Afrika. Nilisafiri Ushelisheli, Kenya, Tanzania na Misri. Nilizungumza na watu wa kawaida huko kwa Kiingereza, Kiswahili, Kifaransa na Kiarabu kidogo. Kabla ya kwenda huko nilijifunza mimi mwenyewe masomo ya Kiafrika. Lakini sikujua sana. Nilidhani Waafrika wanaweza kutofautiana sana nasi kama wageni Wakenya walituambia. Katika kusafiri huko nilitafuta na nimejua kwamba kuna desturi na vitu nyingi kulingana na zetu za Kijapani au za Kiasia Mashariki. |