Karibu Afrika Mashariki


| kurudi Orodhani | Mwisho wa Ukurasa | Uganda | Kenya | Tanzania | Ujapani |

K aribu Ukurasa wa Afrika Mashariki. Ingawa mimi si Mwafrika, ningependa kuwaonyesha watu wowote ulimwenguni mambo ya aina nyingi ambayo ninavyojua juu ya Afrika Mashariki. Kuna sababu kwa nini ninatengeneza huo ukurasa. Ya kwanza ni nilitaka kupatisha ukurasa ulioandikwa na lugha ya Kiswahili. Labda mnajua kuna kurasa nyingi zinazotengenezwa na Watanzania au Wakenya katika Internet, lakini zote zinaandikwa kwa Kiingereza tu. Kwa nini hatumii lugha zao? Kwa hivyo mimi nimekata shauri kuunda ukurasa huu kwa lugha ya Kiswahili, ingawa sijui Kiswahili sana.

Mimi nilipendelea kusafiri kokote ulimwenguni. Nilisafiri nchini nyingi kama Afrika Mashariki, Marekani, Mexico, Ulaya, India na Pakistan, China, Korea na Asia Kusini Mashariki n.k. Nilitembelea mijini kutafuta vitu na kuzungumza na wananchi huko. Watu wowote wanatofautiana na tena kulingana nao, nilivyofundishwa nao. Kama dini gani wangeamini, nyumbani gani wangeishi, tunaweza kuwa marafiki zao ikiwa tunataka kuwa.

Miaka hii sisafiri nchi za kigeni. Kutumia Internet kunaniwezesha kujifunza habari za kigeni bila kwenda huko. Tunaweza kupeleka barua ya Internet kwenda kwa nchi yoyote katika dakika nusu. Tunaweza kupata marafiki zetu ulimwenguni. Nimepata barua kutoka marafiki Waafrika Mashariki pia. Ningependa kujua mambo mengi zaidi juu ya nchi zao, na ningekuwa na furaha nyingi kuwajibu maswali ya aina yoyote wakiniuliza. Kwa hivyo nimetengeneza ukurasa wa mawasiliano. Ningependa kupatia marafiki nyingi ulimwenguni na kujuliana na kuandikiana nao.


UGANDA Kampala
Ubalozi wa Kijapani:
Anwani: 3F. Sheraton Kampala Hotel,
Ternan Avenue, Kampala, Uganda
Posta: S.L.P. 23553, Kampala, Uganda
Simu: (256-41) 347317, 347319
FAX : (256-41) 347348
Ubalozi wa Uganda katika Ujapani:
Anwani: Toukyou-to Shibuya-ku Oyama-chou 39-15,
151 Ujapani
Simu: +81-(0)3-3465-4552
FAX : +81-(0)3-3465-4970
Sijaenda bado Uganda. Kwa hivyo sijui sana juu ya nchi hiyo. Uganda yasemekana kwamba Ufalme wa zamani katika Afrika Mashariki ilikuwako huko. Huo unaitwa Ufalme wa Buganda. Mara moja rafiki yangu alisema kwamba Buganda ilikuwa ina utamaduni wa juu sana ulioendelea huko zamani. Hata sasa kuna vitu vya Buganda vinavyoonekana?
KENYA Nairobi
Ubalozi wa Kijapani:
Anwani: 15F. ICEA Building,
Kenyatta Avenue, Nairobi, Kenya
Posta: S.L.P. 60202, Nairobi, Kenya
Simu: (254-2) 332955, 332956, 332957, 332958, 332959
FAX : (254-2) 216530
Ubalozi wa Kenya katika Ujapani:
Anwani: Toukyou-to Meguro-ku Yakumo 3-24-3,
152 Ujapani
Simu: +81-(0)3-3723-4006, 4007
FAX : +81-(0)3-3723-4488
Kenya yajulikana ni nchi chini ya ikweta, kwa hivyo ukulima wake ni joto jingi sana. Ni kweli kuna joto jingi, nilijua niliposafiri huko. Lakini siyo sana mjini Nairobi. Nairobi iko 1800m juu ya baharini. Kwa hivyo ilikuwa na ukulima wake mzuri sana. Mara nilisikia hata baridi kidogo katika wakati wa kabla ya asubuhi. Mwenyeji Nairobi mmoja aliniambia maana yake Nairobi ni "baridi". Ni kweli? Nilipendelea kukaa Nairobi sana.

Nilisafiri na marafiki zangu kaskazini ya Kenya kwa pikipiki ili kuona wanyama kama vile simba, tembo n.k. Lakini sikuona wao hata kidogo. Niliona punda milia tu. Nilifikiri kabisa hakuna wanyama wengi kasikazini ya Kenya. Ni kweli kuna tembo na simba huko kama mzee mwenyeji huko alituambia "Kuunaa weengii"?


TANZANIA Dar Es Salaam
Ubalozi wa Kijapani:
Anwani: Plot No. 1018, Upanga,
Dar es Salaam, Tanzania
Posta: S.L.P. 2577, Dar es Salaam, Tanzania
Simu: (255-51) 115827, 115829, 115831, 117383, 117384
FAX : (255-51) 115830
Ubalozi wa Tanzania katika Ujapani:
Anwani: Toukyou-to Setagaya-ku Kamiyouga 4-21-9,
158 Ujapani
Simu: +81-(0)3-3425-4531
FAX : +81-(0)3-3425-7844
Kiswahili kimeelea sana Tanzania. Nilisema Kiswahili tu huko katika hotelini, bandarini ya ndege na madukani mengi. Kwa sababu sikuweza kusikia na kusema vizuri, waliniambia polepole. Niliwashukuru sana waliponionyesha njia ya kwenda huku na huko kwa Kiswahili rahisi. Pengine nilifurahi kuzungumza na vijana shuleni ya Dar Es Salaam. Kama ungejua Kiswahili kidogo, ungeelewa utamaduni wa Kiafrika Mashariki vizuri zaidi.

Mjini Dar Es Salaam nilipendelea kula chakula cha aina nyingi cha Kiafrika Mashariki. Baadhi ya chakula ilikuwa ni ya Kihindi kama samosa na chai, ya Kiarabu kama pilau, na ya Kiingereza kama samaki na viazi, au ya mchanganyiko. Sikuzote nilikula matunda mengi na kunywa maji ya matunda mengi pia.


UJAPANI Toukyou

   Hali ya hewa leo katika Ujapani:
Hali ya hewa leo Nilipokuwa mtoto, nilifurahi sana kuangalia sinema ya "Tarzan" kwa televisheni. Kulikuwa na sinema nyingine muhimu ya kuhusu kijana aliyeongoza wanyama katika Afrika, ambayo jina lake nimesahau. Kwa sababu sikuwa na mawasiliano mengi ya Kiafrika, nilikubali hadithi hizo ni kweli. Nilidhani wanyama na misitu zinaenea mahali popote katika bara Afrika, hadi nilikuwa nimekuwa mwanafunzi wa chuo kikuuni wakati ambapo niliona wageni kutoka Afrika kwa mara ya kwanza.

Wageni hao walikuwa wanafunzi Wakenya. Labda walikaribishwa na serikali ya Kijapani wakakuja na wakaishi huku kwa muda. Siku moja walikuja chuo kikuuni chetu na walituonyesha kucheza ngoma na nyimbo nzuri za Kenya. Baadaye walituambia mambo fulani juu ya Kenya na Afrika Mashariki kwa Kiingereza. Nilikuwa na nafasi nzuri ya kuzungumza nao, lakini sikuweza kusema maneno hata kidogo. Vijana Wajapani wengine wengi walikuwa pia ni kimya tu. Wakenya wote walisema mengi. Kwa hivyo walionekana walifikiria kwamba sisi vijana Wajapani hatujui Kiingereza au hatuna neno katika mazungumzo na wageni. Lakini si kweli.

Wageni hao walitueleza kwamba watu wa Afrika Mashariki wanaelekea utamaduni wa Kizungu hasa wa Kiingereza. Kwa hivyo utamaduni wa Kijapani au Kiasia ulionekana kwao ni ya kigeni sana. Walisema wanatofautiana na Wajapani mahali popote wakati kokote. Maana yake ni hawakupendelea kukaa huku Ujapani wakila chakula cha Kijapani, wakisikilia muziki ya Kijapani au wakiona picha ya Kijapani.

Miaka fulani baadaye nilitembea bara Afrika. Nilisafiri Ushelisheli, Kenya, Tanzania na Misri. Nilizungumza na watu wa kawaida huko kwa Kiingereza, Kiswahili, Kifaransa na Kiarabu kidogo. Kabla ya kwenda huko nilijifunza mimi mwenyewe masomo ya Kiafrika. Lakini sikujua sana. Nilidhani Waafrika wanaweza kutofautiana sana nasi kama wageni Wakenya walituambia. Katika kusafiri huko nilitafuta na nimejua kwamba kuna desturi na vitu nyingi kulingana na zetu za Kijapani au za Kiasia Mashariki.


| kurudi Orodhani | Mwisho wa Ukurasa | Uganda | Kenya | Tanzania | Ujapani |

Kuniandikia barua ya Email: kwa NH
Ilitengenezwa na NH, Kawasaki 1997. Asante.