asa karibu wote wa vijana na watoto Wajapani wamekuwa wanafundishwa kutumia kompyuta katika shuleni. Kompyuta zina wekwa shuleni za msingi (miaka sita) kwa asilimia 100%. Katika shuleni za sekondari (miaka tatu) wanafunzi wanatazamiwa kutumia software kama wordprocecessing, database, painting and drawing na hesabu yenye tables. Wanafunzi wa shuleni za sekondari juu (miaka tatu) au wa vyuo vikuuni (miaka minne) wanafikiriwa kujua sana. Baadhi yao wanafunzi wanaweza kuandika program fulani au kurasa za nyumbani za Internet na kadhalika.
Leo inatazamiwa kuwa kampuni na afisi kubwa zote zina kompyuta. Katika baadhi ya kampuni na afisi, wafanyakazi wanatumia kompyuta sikuzote wakiandika barua, wakihesabia na wakipatia habari. Ni kweli katika kampuni yangu iitwayo "Gakken" afisi nyingi zina kompyuta, hata kompyuta moja kwa mfanyakazi mmojo. Maana yake wafanyakazi wengi wanajua kutumia kompyuta, lakini si wote. Wasiojua au wasiotaka kutumia kompyuta ambao wengi ni wazee wanafanya kazi kama walivyofanya kwa muda mrefu. Vijana wafanyakazi ni lazima wajue mafunzo ya mawasiliano na kutumia kompyuta na mashine ya kisasa.
Katika nyumbani Wajapani asilimia 35% au 40% kuna kompyuta. Idadi ya kompyuta zaidi ya milioni mbili zinauzwa kila mwaka huku. Kwa hivyo kuna mamilioni ya watumiaji wa kompyuta na wasafiri wa Internet katika Ujapani. Kuna Internet providers nyingi sana pia hapa, labda zaidi ya elfu mbili.